; Kongamano la Biashara na Uwekezaji ROME, Italia Tarehe 4-5 MEI, 2017. » Tanzania Tourist Board
 
Language English Kiswahili

Kongamano la Biashara na Uwekezaji ROME, Italia Tarehe 4-5 MEI, 2017.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kinaratibu kongamano la biashara na uwekezaji ‘Tanzania Day’ baina ya Tanzania na Italia litakalofanyika tarehe 4-5 Mei, 2017, Rome, Italia. Lengo la kongamano hili ni kuwakutanisha ana kwa ana wafanyabiashara/wawekezaji wa nchi hizi mbili ili kujadiliana fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji zitakazowezesha kuanzisha na kuendeleza miradi ya viwanda, kupata wabia wa kuleta mitaji ya biashara, tekinolojia pamoja na kupata masoko.

 

Sekta zilizolengwa ni miundombinu; usafirishaji; viwanda vya kusindika mazao ya kilimo; viwanda vya mvinyo; viwanda vya kuzalisha madawa; kilimo cha viungo; kutengeneza meli na magari; viwanda vya kuchakata nyama; utalii; uvuvi; ujenzi wa majengo; usindikaji wa asali; utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na ngozi na pamba; kuchimba na kuongeza thamani madini.

Tunategemea Tanzania itaongeza thamani ya mitaji ya uwekezaji kutoka nje (FDI) iwapo makampuni ya wafanyabiashara kutoka Italia na Tanzania  yatakubaliana  kufanya biashara na kuwekeza Tanzania. TIC inapenda kutumia fursa hii kuwatangazia wafanyabiashara nchini kushiriki kongamano hili.

 

Wafanyabiashara watakaopenda kushiriki kongamano hili watahitajika kujiandikisha TIC kabla ya tarehe 20 Machi, 2017. Aidha washiriki wa kongamano watahitajika kujigharamia usafiri na malazi ya kwenda Italia. Programu ya kongamano itatumwa kwa washiriki mara baada ya kuthibitisha ushiriki wao. Wafanyabiashara watakaopenda kushiriki wathibitishe ushiriki wao kwa (Bi. Latiffa Kigoda simu. 0715734444 /latiffa.kigoda@tic.co.tz) au (Bw. Ayoub Magarya simu no. 0654862931/ ayoub.magarya@tic.co.tz).

IMETOLEWA NA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA

 

 

Contact Information

Contacting us by post Tanzania Tourist Board
Utalii House - Laibon street/Ali Hassan Mwinyi Road - Opposite French Embassy
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email md@tanzaniatouristboard.go.tz
Contacting us by telephone
General: +255 22 2664878/9
Marketing:+255 22 2664875
Tourism Services:+255 22 2664873
Information Center:+255 22 2131555
  • Branch Offices
  • Contacting us by fax

    Did you know!

    The Kipunji also known as the highland Mangabey, is a species of old world monkey which is only found in the highland forest of Tanzania.

    S!TE 2017 PARTICIPANTS COMMENTS